Jumatatu 18 Agosti 2025 - 11:51
Kikao maalumu na wanafunzi wa Tanzania, Malawi na Burundi chafanyika Qum Irani, kikiwa na maudhui ya kumkuza mwanafunzi katika ngazi ya kutumia fani mbali mbali za kisasa

Hawza/ Wanafunzi wa Tanzania, Malawi na Burundi wakutana na wakili wa Jaamiatul-Mustafa pamoja na Raisi wa Taasisi ya Bayani ili kujadili jinsi ya kuweza kumkuza mwanafunzi hasa hasa katika kutumia kutumia fani mbali mbali za kisasa kama vile akili mnemba

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, leo siku ya jumatatu sawa na tarehe 18/ 8/ 2025 wanafunzi wa nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Burundi na Mawali wamekutana na wakili wa Jaamiatul Mustafa katika nchi hizo na kuweza kujadiana mambo kadhaa ambayo yalikuwa yakibainisha mustakbali wa wanafunzi ambao bado wanasoma katika mji wa Qum Iran, katika kikako hicho Dkt. Ali Taqawi alianza khutuba yek kwa kukumbuka dhulma ambazo amefanyiwa bwana wa Mashahidi Imam Hussein (as), kwa kusoma riwaya isemayo:


 ان لقتلى الحسين حرارة في قلوب المؤمنين لا تبرد ابدا 

Kwa kunukuhu riwaya hii Dkt. Taqawi alielezea uzito wa shahada ya Imam Hussein juu ya wafuasi wa madhehebu ya Ahlubayt (as) na kusema kwamba, hakuna mtu yeyote atakaye weza kuifuta athari ya Imam Husein kwenye nyoyo za waumini wa Kishia.

Katika muendelezo wa khutuba yake Dkt. Taqawi aliwahusia wanafunzi waliopo katika mji wa Qum Iran, kwa kusema:

Wanafunzi kando na kusoma masomo ya dini wanatakiwa waweke bidii zaidi katika fani mbali mbali na kusema: Dunia ya sasa imesonga mbele sana kiasi cha kwamba mwanafunzi wa dini yampasa awe ni mwenye kumiliki fani mbali mbali, katika kulielezea hilo kwa bayana amesema watu wengi wamekuwa wakitaka kufungua madrasa za Qur'ani, kisha akasema hiyo ni fikra nzuri sana, lakini kando na kufungua Madrasa ya Qur'ani inatakiwa mtu awe na fani nyingine tofauti.

Katika kusisitisa umuhimu wa Qur'ani Dkt. Taqawi alisema: Moja ya vitu ambavyo mashia bado wapo nyuma ni kuhusiana na kuhifadhi Qur'ani tukufu, katika hilo alisisitiza sana wanafunzi wawekeze bidii zaidi kwenye kuhifadhi Qur'ani na kusema kwamba; yupo tayari kumkingia kifua mwanafunzi yeyote ambae atakuwa tayari katika kufanikisha zoezi hili au fani nyengine yeyote ile, alitolea mifano tofauti katika hilo na kusema kwamba watu wajitahidi kutumia nafasi hii waliyo pewa.

Kikao maalumu na wanafunzi wa Tanzania, Malawi na Burundi chafanyika Qum Irani, kikiwa na maudhui ya kumkuza mwanafunzi katika ngazi ya kutumia fani mbali mbali za kisasa

BAadhi ya Masheikh ambao walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu zaidi kikao hicho

Katika mwendelezo wa kikao hicho pia watu wengine walipata nafasi ya kutoa nadharia zao akiwemo, Raisi wa Taasisi ya Bayani Dkt. Barar Puur, na Dkt. Yaq'ubi ambae anatajruba ya kufanya kazi katika nchi mbali mbali za Afrika kwa zaidi ya miaka 40, na wote hao waliweza kuelezea tajruba mbali mbali walizo kutana nazo pamoja na changamoto mbali mbali.

Kikao maalumu na wanafunzi wa Tanzania, Malawi na Burundi chafanyika Qum Irani, kikiwa na maudhui ya kumkuza mwanafunzi katika ngazi ya kutumia fani mbali mbali za kisasa

Mashekh wengine ambao na walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu zaidi kikao hicho

Mwisho wa kikao hicho Raisi wa Taasisi ya Bayani Dkt. Barar Puur, aliezea fani mbali mbali ambazo zinafundishwa katika Taasisi hiyo na kuwataka wanafunzi wa Jaamiatul-Mustafa kutumia fursa hiyo kwani ni lulu adimu sana kwao, na akasema kuwa kuna watu wengi ambao walitamani nao wajiunge na nyinyi hapa Irani lakini hawakuweza kuipata fursa hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha